Psalms 112

Baraka Za Mwenye Haki


1
Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
bMsifuni Bwana.

Heri mtu yule amchaye Bwana,
mtu yule apendezwaye sana na amri zake.


2 cWatoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi,
kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.

3 dNyumbani mwake kuna mali na utajiri,
haki yake hudumu milele.

4 eHata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu,
yule mwenye rehema, huruma na haki.


5 fMema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba,
anayefanya mambo yake kwa haki.

6 gHakika hatatikisika kamwe,
mtu mwenye haki atakumbukwa milele.

7 hHataogopa habari mbaya,
moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana.

8 iMoyo wake ni salama, hatakuwa na hofu,
mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake.

9 jAmetawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini;
haki yake hudumu milele;
pembe yake itatukuzwa kwa heshima.


10 kMtu mwovu ataona na kuchukizwa,
atasaga meno yake na kutoweka,
kutamani kwa mtu mwovu kutaishia patupu.
Copyright information for SwhKC